"Wahadhiri wanaozungumza Kifaransa wameendesha duru ya sasa ya warsha iliyofanyika kuanzia Agosti 7-11 na washiriki wametunukiwa vyeti baada ya kukamilisha warsha", alisema Naibu wa Masuala ya Kimataifa katika kitengo Elimu na Utamaduni chaidara hiyo , akibainisha kuwa wanafunzi 35 wa Madagascar na wanaharakati walishiriki.
Kwa mujibu wa Seyyed Mohammad Zolfaghari, aina mbalimbali za programu ziliangaziwaa katika duru hii ya warsha kama vile kozi za mafunzo, kutembelea maeneo mbali mbali ya Haram, kushiriki katika maombolezo ya Muharram, mafunzo kuhus maisha na mwenendo wa Imam Hussein AS.
Alitaja lengo la duru ya hivi karibuni ya warsha kuwa ni kujua maisha na mwenendo wa Imam Ridha AS, shughuli za kielimu na kitamaduni na uwezo wa Haram, kuanzisha uhusiano mzuri na vituo vya kitamaduni na wanaharakati, na kuwawezesha wapanue mtandao wao wa kimataifa.
Ameongeza kuwa warsha hizo za hivi karibuni pia zililenga kuwafahamisha washiriki mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. "Tunatumai kwamba wanafunzi hawa wachanga na wanaharakati wa kitamaduni wanaweza kuleta madiliko chanya barani Afrika katika siku zijazo".
3480049