IQNA

Ustawi wa Uislamu

Misikiti mipya 200 inahitajika Morocco kila mwaka

18:24 - October 21, 2022
Habari ID: 3475961
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa masuala ya Kiislamu wa Morocco alisema nchi hiyo inahitaji kujenga misikiti 200 kila mwaka.

"Ujenzi wa misikiti mipya unalenga kwenda sambamba na ukuaji wa idadi ya watu nchini na upanuzi wa miji," Ahmed Toufiq alisema wakati wa maadhimisho ya Siku ya Misikiti katika mji mkuu wa Morocco wa Rabat.

Wizara yake inataka kujenga "misikiti 80 katika miaka mitano ijayo," aliongeza, akitoa wito kwa wafadhili "kuunga mkono serikali katika kujenga misikiti 1,000 katika kipindi hicho cha miaka mitano."

"Kwa sasa kuna jumla ya misikiti 2,216 iliyofungwa, 723 kati yake iko katika mchakato wa ukarabati ili kufunguliwa," Toufiq alidokeza.

Kuna misikiti 51,000 nchini Morocco, asilimia 72 ambayo iko mashambani, waziri huyo alibainisha.

3480933

captcha