IQNA

Harakati ya Qur'ani Tukufu

‘Siku ya Qur'ani Tukufu’ yapangwa nchini Iraq

21:37 - February 07, 2023
Habari ID: 3476529
TEHRAN (IQNA) - Taasisi za Qur'ani nchini Iraq zinashinikiza nchi hiyo kuitaja siku moja katika kalenda kuwa 'Siku ya Qur'ani Tukufu.'

Shinikizo hilo ni  sehemu ya Siku ya Qur'ani Tukufu Duniani, kampeni iliyoanzishwa na Idara ya Mfawidhi wa Haram  Takatifu ya Imam Hussein (AS) nchini Iraq, inayolenga kukuza mafundisho ya Qur'ani Tukufu na kutafakari kuhusu aya zake.

Idara ya Mfawidhi wa Haram  Takatifu ya Imam Hussein (AS) iliandaa kikao cha kamati ya maandalizi ya Siku ya Qur'ani Tukufu Duniani siku ya Jumapili ili kujadili maandalizi ya kuandaa programu katika hafla hiyo.

Sheikh Hassan al-Mansouri, Idara ya Mfawidhi wa Haram  Takatifu ya Imam Hussein (AS) amesema washiriki wa mkutano huo wamesisitiza haja ya kuwepo ushirikiano baina ya vyombo vyote vya Qur'ani Tukufu Iraq kwa ajili ya kuandaa hafla hiyo kikamilifu.

Mnamo Machi 2020, Idara ya Mfawidhi wa Haram  Takatifu ya Imam Hussein (AS) ilitangaza Eid al-Mabath (siku ambaye Mtume Muhammad (SAW) aliteuliwa kutuma ujumbe wa Mwenyezi Mungu) kama Siku ya Qur'ani Tukufu Duniani.

Mansouri alisema wakati huo kwamba malengo ya kutangaza siku moja kuwa siku ya Qur'ani duniani ni pamoja na kustawisha umoja katika Umma wa Kiislamu na kuwafahamisha wafuasi wa dini nyinginezo kitabu hicho Kitukufu.

4120057

Kishikizo: qurani tukufu iraq
captcha