IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Hatua ya awali ya Mashindano ya Qur'ani kwa Wakimbizi wa Afghanistan nchini Iran

19:55 - February 17, 2023
Habari ID: 3476574
TEHRAN (IQNA) - Hatua ya awali ya mashindano ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya wakimbizi wa Afghanistan wanaoishi nchini Iran ilifanyika katika mji mtakatifu wa wa Qom nchini Iran ambapo kulikuwa na washiriki 370.

Hafla hiyo imeandaliwa na tawi la Qom la Kituo cha Kimataifa cha Kustawisha Qur'ani Tukufu, chenye uhusiano na Mfawishi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) nchini Iran, na Kituo cha Qur’ani Tukufu cha Shahid Habib ibn Muzahir cha Kuwait.

Kulingana na waandalizi, wakimbizi wa Afghanistan wanaoishi katika miji mbalimbali ya Iran walishiriki katika shindano hilo lililofanyika kwa njia ya intaneti.

Montazer al-Mansouri, mkuu wa kituo hicho, alisema kuwa mashindano hayo yanajumuisha kategoria tofauti ikiwa ni pamoja na usomaji wa Tahqiq, Tarteel, ufahamu wa Qur'ani, na tafsiri ya Sura Al-Hujurat kwa wanaume na wanawake wenye umri wa juu na chini ya miaka 16.

Washiriki watano katika kila kategoria wamefanikiwa kutinga fainali ya shindano hilo ambalo baadaye litafanyika kibinafsi katika mji mtakatifu wa Qom.

Kulingana na mipango, hii ni toleo la pili la shindano.

Iran imekuwa ikihifadhi wakimbizi wa Afghanistan tangu mwishoni mwa miaka ya 1970 wakati nchi hiyo ilipovamiwa na Jeshi la Shirikisho la Sovieti na kisha ikavamiwa na Marekani  na waitifaki wake wa NATO mwaka 2001. Ingawa wengi wa wakimbizi hao wamerejea nchini mwao kwa hiari, bado kuna mamilioni ya wakiimbizi  Waafghanistan nchini Iran ambao wanapewa suhula zote wanazohitajia katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4122672
captcha