IQNA

Sherehe za kufunga Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran

TEHRAN (IQNA)- Jumatano kumefanyika sherehe ya kufunga Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu, ambapo washindi walitangazwa na kutunukiwa tuzo. Sherehe hiyo imehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyed Ebrahim Raisi na halikadhalika Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Mohammad Mehdi Esmaeili, na Waziri wa Elimu Yousef Nouri.