IQNA

Khums katika Uislamu /5

Faida za Kulipa Khums

21:52 - November 07, 2023
Habari ID: 3477857
TEHRAN (IQNA) – Kuna nukta nyingi zilizotajwa ndani ya Qur'ani Tukufu na Hadithi kuhusu faida za kulipa Khums.

Baadhi ya nukta hizi kuhusu Khums katika Uislamu ni kama zifuatazo:

  • Kizazi Kisafi

Kwa mujibu wa Hadithi, kulipa Khums kutatakasa mali ya mtu na huo ni utangulizi wa kuwa na kizazi kilichotakasika.

  • Kuimarisha dini

Imam Ridha (AS) alisema kwamba Khums ni haki ya Ahl-ul-Bayt (AS), yaani watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (SAW)  na ni usaidizi wa njia na mafundisho yao.

  • Ishara ya kujitolea

Tunasoma katika Hadithi nyingine kwamba Mwislamu wa kweli ni yule ambaye ameshikamana na ahadi yake kwa Mwenyezi Mungu na kwamba mwenye kutamka kwa  ulimi wake imani lakini imani hiyo haiku moyoni basi si Mwislamu wa kweli.

  • Kusaidia marafiki

Imamu Ridha (AS) alisema Khums ni njia ambayo kwayo tunasaidia jamaa na marafiki zetu.

  • Usafi wa mali

Imamu Sadiq (AS) alisema kwamba kwa kuchukua dirham kutoka kwa watu (kama Khums), hana nia nyingine zaidi ya kutakasa pesa zao.

  • Kufanya kipato kuwa kitamu

Katika Hadith nyingine, Imamu Sadiq (AS) alisema kwamba yeyote anayelipa Khums, mapato yake mengine yatakuwa matamu kwake.

  • Kulinda sifa dhidi ya wapinzani

Imam Ridha (AS) alisema kwamba Khums husaidia kulinda sifa ya wafuasi wa Ahl-ul-Bayt (AS.

  • Kuondoa umasikini kutoka kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (SAW)

Imam Kadhim (AS) alisema kwamba Mwenyezi Mungu ameweka nusu ya Khums kwa ajili ya kuwaondolea umasikini kizazi cha Mtukufu Mtume (SAW) ambao hawawezi kunufaika na Zaka na Sadaka.

  • Ni Fidia ya madhambi na hifadhi ya Siku ya Kiyama

Imamu Ridha (AS) alisema kwamba kulipa Khums kutoka kwenye pesa za mtu kunasababisha kusamehewa madhambi yake na itakuwa ni hifadhi ya Siku ya Kiyama.

  • Dhamana ya peponi

Mtu mmoja alikwenda kwa Imam Baqir (AS) na akalipa Khums zake. Imam (AS) alisema ni muhimu kwani itamdhaminia mtu huyo pepo.

  • Kupokea maombi ya Maimamu watoharifu

Imamu Ridha (AS) amesema: “Khums inatusaidia katika kuhifadhi itikadi ya (Ahl-ul-Bayt).” Kisha akasema: “Msijaribu kujinyima nafsi zenu na maombi yetu kadri mwezavyo.”

  • Ufunguo wa riziki

Imam Ridha (AS) alisema: “Kulipa Khums ni ufunguo wa riziki yako.”

  • Utaratibu na nidhamu katika mtaji wa mtu

Mwenye kuhesabu Khums zake na kuzilipa kila mwaka, ni mtu mwenye utaratibu na nidhamu.

Imam Baqir (AS) amesema: “Ukamilifu wa hali ya juu ni katika mambo matatu: Kuwa na elimu ya kina ya dini, uthabiti katika kukabiliana na matatizo, na kuwa na utaratibu na mipango katika maisha.

  • Baraka maalum

Wale wanaolipa Khums hakika watapata usikivu maalum na baraka za Mungu.

Qur'ani Tukufu inasema, “Basi nikumbukeni Mimi, nitakukumbukani”? (Aya ya 152 ya Surah Al-Baqarah)

Qur'ani Tukufu inasema, “Ukifanya wema, itakuwa kwa faida yako mwenyewe”? (Aya ya 7 ya Suratul Israa)

Qur'ani Tukufu inasema: “Na mnapoamkiwa kwa maamkio, basi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu,” (Aya ya 86 ya Surat An-Nisaa)

Qur'ani Tukufu inasema: “Enyi Waumini, kama mkimnusuru Mwenyezi Mungu, atakunusuruni na atakuwekeni imara (katika imani yenu)” (Aya ya 7 ya Surah Muhammad)

Qur'ani Tukufu inasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wafanyao wema”? (Aya ya 195 ya Surah Al-Baqarah)

Hivyo atakayelipa Khums atajumuishwa miongoni mwa wale ambao aya zilizotajwa hapo juu zinawahusu.

Kishikizo: khums
captcha