Vigezo vitano vinavyotolewa na wanachuoni kwa madhambi makubwa ni kama vifuatavyo:
1- Dhambi yoyote ambayo Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu ameahidi adhabu juu yake.
2- Dhambi yoyote ambayo Uislamu umeichukulia kuwa ni Hadd, kama vile kunywa mvinyo, zinaa n.k.
3- Dhambi yoyote inayoonyesha kudharau dini.
4- Dhambi yoyote iliyothibitishwa kwa dalili wazi kuwa ni Haramu na kubwa.
5- Dhambi yoyote ambayo Qur'ani na Sunnah imewaonya vikali wanaoifanya.
Kuhusu idadi ya madhambi makubwa, kumetajwa idadi tofauti, ikiwa ni pamoja na 7, 10, 20, 34 na 40.
Kwa mujibu wa kitabu, Tahrir al-Wasilah cha Imam Khomeini (RA), madhambi makubwa ni mengi, nayo ni pamoja na:
1- Kupoteza matumaini katika rehema za Mwenyezi Mungu
2- Kujisikia umesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu
3- Kunasibisha maneno yasiyo ya kweli kwa Mwenyezi Mungu, Mtume (SAW) na Maasumin (AS)
4- Mauaji
5- Kutowaheshimu wazazi
6- Kula mali za mayatima
7- Kukashifu wanawake wasio na dhambi
8- Kutoroka vitani
9- Kukata mahusiano ya kifamilia
10- Uchawi
11- Uasherati
12- Maingiliano ya jinsia moja
13- Wizi
14- Kuapa kwa uwongo
15- Kuficha ushuhuda
16- Kutoa ushahidi wa uongo
17- Kuvunja ahadi
18- Kutenda kinyume na mapenzi ya mtu
19- Kunywa mvinyo
20- Riba
21- Kula mali iliyopatikana kwa njia za Haramu
22- Kamari
23- Kula maiti za wanyama na kunywa damu
24- Kula nyama ya nguruwe
25- Kula nyama ya mnyama ambaye hajachinjwa kwa mujibu wa sheria ya dini
26- Kupunguza mizani wakati wa kuuza bidhaa
27- Kuhama kwenda mahali ambapo mtu atapoteza dini yake
28- Kuwasaidia madhalimu
29- Kuwategemea madhalimu
30- Kujiwekea haki za wengine
31- Uongo
32- Kiburi
33- Ufujaji
34- Upotovu
35- Kusengenya
36- Kupelekeza mambo ya wengine
37- Kujishughulisha na tafrija na pumbao nyingi
38- Kupuuza Hijja
39- Kuacha Salah
40- Kutotoa Zaka
41- Kusisitiza kufanya madhambi madogo.
Na bila shaka Shirki (ushirikina), kukataa aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na uadui na watu wa Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa madhambi makubwa.