IQNA

Jiografia ya Matukio katika Qur'ani Tukufu/3

Adamu na Hawa walishukia wapi kwa mara ya kwanza?

15:58 - December 14, 2023
Habari ID: 3478032
IQNA - Watu wote waliowahi kuishi duniani ni kizazi cha Adam (AS) na Hawa.

Baada ya Adamu na Hawa kula tunda walilokatazwa, Mwenyezi Mungu aliwafukuza kutoka peponi kwa sababu ya kutotii kwao na hivyo wakashuka duniani.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 36-38 ya Sura Al-Baqarah: Lakini Shet'ani aliwatelezesha hao wawili na akawatoa katika waliyo kuwamo, na tukasema: Shukeni, nanyi ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Katika ardhi yatakuwa makaazi yenu na starehe kwa muda. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu.  Tukasema: Shukeni nyote; na kama ukikufikieni uwongofu utokao kwangu, basi watakao fuata uwongofu wangu huo haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika. 

Sasa swali ni je, Adamu na Hawa walishukia wapi kwa mara ya kwanza kabisa walipofika duniani?

Kuna maoni mbalimbali juu ya suala hili, mawili makubwa yakiwa yafuatayo:

1- Mlima Sarandib katika Sri Lanka ya leo. Katika Hadith nyingi, Mlima Sarandib nchini Sri Lanka unatajwa kuwa mahali pa Hubut (kushukia) na makazi ya kwanza ya Adam (AS). Katika kisiwa hiki kuna mlima ambao Wareno wameuita Adam's Peak na juu yake kuna mabaki ya nyayo za Adamu. Mlima huo una urefu wa futi 7,420 na inasemekana kwamba mimea inayoota kwenye mlima huu ililetwa na Adamu kutoka peponi. Waislamu, Wakristo na Wabudha wanatembelea eneo ambalo mabaki ya nyayo hizo ziko kwenye mwamba juu ya mlima.

Msafiri maarufu wa Morocco Ibn Battuta alitembelea kisiwa hicho, ambako watu bado wanawaita Adam (AS) baba na Hawa mama.

Kwa mujibu wa Hadith, mmoja kati ya Maimamu Maasumu (AS) ameielezea Sarandib kuwa ni sehemu bora zaidi duniani ambapo Adam (AS) alishuka kutoka peponi.

2- Milima ya Safa na Marwa. Katika baadhi ya Hadithi, Milima ya Safa na Marwa inatajwa kuwa ni sehemu ambayo Adam na Hawa walishukia.

Ni milima miwili ya chini upande wa mashariki wa Msikiti Mkuu huko Makka. Kwa mujibu wa maelezo ya kihistoria, Hagar, mke wa Nabii Ibrahim (AS) alijaribu kumtafutia maji mtoto wake Ismail (AS) katika eneo la kati ya milima hii miwili. Mlima Safa palikuwa mahali ambapo Mtume Muhammad (AS) alianza kueneza Uislamu hadharani.

 

Kishikizo: qurani tukufu adam hawa
captcha