IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Palestina ni kadhia muhimu katika Umma wa Kiislamu

19:34 - December 22, 2023
Habari ID: 3478076
IQNA-Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema kuwa Palestina ndiyo kadhia muhimu zaidi ya Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa: Leo hii harakati ya Muqawama ndiye mshindi halisi.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Kazem Siddiqui amesisitiza katika hotuba za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran kuwa, Umma wa Kiislamu unapaswa kuikomboa Palestina kutoka mikononi mwa Wazayuni maghasibu na kusema: "Sababu kuu ya jinai zinazofanyika katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni Marekani na nchi nyingine za Magharibi, zikiwemo Uingereza na Ufaransa."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran ameeleza kuwa, mrengo wa nchi za Magharibi daima hufanya njama za kuua, kufanya mapinduzi na kuanzisha vita na kuongeza kuwa: "Leo hii kambi ya Magharibi hususan Wazayuni imejikita katika kuendeleza uvamizi, lakini wameshindwa kukabiliana na hamasa ya kijeshi na mujahidina wa kundi moja."

Hujjatul-Islam Wal Muslimin Siddiqui ameongeza kuwa: "Uingereza, Ufaransa na Marekani sinashiriki katika jinai na uhalifu wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza."

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa, Marekani na mrengo wa Magharibi haujawahi kutengwa na kuchukiwa zaidi kama ilivyo hivi sasa na kuongeza kuwa: "Leo hii wananchi wa Marekani wameamka na wale wanaodai kutetea uhuru hawawaruhusu wananchi na wasomi kutoa maoni yao."

Hujjatul-Islam Siddiqui amesema: "Leo mapambano ya Kiislamu (Muqawama) yamebadilisha milingano ya nguvu haswa watu shupavu na mashujaa wa Yemen ambao wamechukua hatua madhubuti katika mkondo huo wa Muuqawama."

4189296

captcha