IQNA

Harakati za Qur'ani

Waislamu nchini Brunei wauaga mwaka 2023 kwa Khitmah ya Qur'ani Tukufu

14:50 - January 01, 2024
Habari ID: 3478126
IQNA – Kikao cha Khitmah ya Qur'ani Tukufu (kusoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho) kimefanyika katika msikiti mkubwa huko Brunei kuashiria mwisho wa mwaka wa 2023.

Waumini wa Msikiti wa Hassanal Bolkiah huko Kampong Mentiri, Brunei, waliukamilisha mwaka wa 2023 kwa hafla ya Khitmah siku ya Jumapili.

Mkutano huo wa kimaanawi ulifanyika katika makazi ya kiongozi wa kikundi cha wasomaji wa Qur'ani Tukufu, Haji Zainal bin Haji Ghani, kuashiria mwisho wa mwaka wa Miladia ambapo washiriki kwa pamoja walisoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho,  amali ambayo ni muhimu katika imani ya Kiislamu.

Kikao kilianza kwa washiriki kujishughulisha na usomaji wa Qur'ani Tukufu punde baada ya Sala ya Alfajiri. Mmoja wa washiriki alisisitiza jukumu la Qur'ani Tukufu kama chanzo cha mwanga na mwongozo katika maisha ya kila siku.

Mtazamo huu unaendana na mfumo mkubwa wa imani ya Kiislamu ambao unaiona Qur'ani Tukufu kama nuru inayoongoza, inayotoa suluhisho kwa matatizo ya kidunia na kutumika kama dira ya maadili na akhlaqi.

3486634

Kishikizo: brunei qurani tukufu
captcha