IQNA

Rais Hassan Rouhani

Nchi za Kiislamu ziungange kuwasaidia Wapalestina Ghaza

10:40 - July 11, 2014
Habari ID: 1428175
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe kwa viongozi wa nchi zote za Kiislamu duniani na kusisitiza kwamba ulimwengu wa Kiislamu unapasa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha unakomesha haraka iwezekanavyo mzingiro wa kidhulma uliowekwa na Wazayuni dhidi ya wananchi wa eneo la Ukanda wa Ghaza

Aidha ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuwasaidia wananchi wa Palestina ambao hivi sasa wanakabiliwa na wimbi la mashambulio ya anga ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Rais Hassan Rouhani ameongeza kuwa, hivi sasa unahitajika umoja na mshikamano zaidi wa umma wa Kiislamu kuliko wakati mwingine wowote na kusisitiza kwamba, mwendelezo wa mzingiro wa kidhulma dhidi ya wananchi wa Ghaza na ukosefu mkubwa wa chakula, dawa na suhula nyingine za tiba unaweza kusababisha kutokea maafa makubwa ya kibinadamu katika eneo hilo.
Rais Rouhani amesisitiza kuhusu kupelekwa misaada kwa wananchi madhulumu wa Palestina na kusimamishwa vitendo vya kichokozi vya utawala wa Israel, ni jukumu la pamoja la taasisi, mashirika yote ya kimataifa na nchi zote huru duniani. Rais wa Iran ameuelezea muqawama wa wananchi wa Palestina dhidi ya uchokozi wa adui Mzayuni na kusisitiza kwamba, utawala wa Israel kwa mara nyingine utashindwa mbele ya irada na azma ya wanamapambano wa Kiislamu wa Palestina.
Utawala haramu wa Israel unaendeleza hujuma zake dhidi ya Ukanda wa Ghaza ambapo idadi kubwa ya Wapalestina waliouawa shahidi ni wanawake na watoto. Hadi kufikia sasa idad Wapalestina waliouawa shahidi katika hujuma za ndege za kivita za utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo lililozingirwa la Ukanda wa Ghaza imeongezeka na kufika zaidi ya 96 na zaidi ya 700. Ndege za utawala haramu wa Israel zimeshambulia maeneo 600 katika eneo hilo la Palestina katika kipindi cha siku tatu zilizopita.

1428142

captcha