IQNA

Wasomi Waislamu

Ibn al-Jazari; Msomi mkubwa wa Qari na Qur'ani Tukufu

20:17 - December 03, 2023
Habari ID: 3477979
TEHRAN (IQNA) – Jumamosi iliadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Ibn al-Jazari, qari mashuhuri katika karne ya 14 na 15 Miladia ambaye pia alikuwa mwanachuoni mashuhuri wa sayansi ya Qur’ani.

Abu al-Khayr Shams al-Din Muhammad bin Muhammad bin Muhammad bin Ali bin Yusuf al-Jazari (Novemba 1350 – Disemba 1429) alikuwa mwanazuoni katika fani ya Qira’at ya Qur’ani, ambaye al-Suyuti alimchukulia kama “ mamlaka ya juu kabisa ya mambo haya".

Pia alikuwa ni mtaalamu katika fani ya Hadithi, akiandika kitabu mashuhuri katika uwanja huu kwa jina la “Al-Hidaya fi Ilm al-Riwaya”.

Alizaliwa na kukulia Damascus, ingawa nisba (jina la sifa), Jazari, linaashiria asili ya Jazirat ibn Umar katika Uturuki ya leo.

Alihifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 13 na alisoma Qira’at na Tajweed pamoja na wanazuoni wakubwa katika fani hii kisha akawa qari kubwa.

Pia alijifunza Tafsir (Tafsiri ya Qur'ani ), Fiqh, Hadithi, Usul, Balagha, n.k.

Ibn al-Jazari alihudumu katika nyadhifa nyingi za kidini na mahakama pamoja na kufundisha katika Msikiti wa Bani Umayya huko Damascus.

Alihudumu kama hakimu au kadhi mkuu katika jiji la Shiraz, Iran, kwa miaka michache.

Pia alianzisha shule za Qur'ani Damascus na Shiraz.

Ibn al-Jazari aliandika vitabu vingi katika nyanja za Quran, Hadith, Seerah ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na historia ya Uislamu.

Alifariki mwaka wa 833 Hijria (1429) huko Shiraz akiwa na umri wa miaka 82 na akazikwa katika Shule ya Dar-ul-Quran aliyokuwa ameianzisha.

3486260

captcha