Abdelaziz Djerad amesema kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya na madaktari, haiwezekani kufungua misikiti ya nchi hiyo ambayo ilifunguwa mwezi Machi ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19.
“Pundu ugonjwa wa corona utakapoangamizwa, basi sote tutaswali pamoja swala ya jamaa katika misikiti,” amesema Waziri Mkuu Dejrad.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na miito ya kutaka misikiti ifunguliwe.
Hadi kufikia sasa watu 14,272 wameambukizwa corona nchini Algeria huku wengine 920 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo unaozidia kuenea kwa kasi kote duniani.