IQNA

Kituo cha Harvad Marekani: Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi

17:37 - March 20, 2022
Habari ID: 3475058
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kimataifa ya Haki za Kibinadamu cheye makao yake makuu nchini Marekani katika Chuo Kikuu cha Sherai cha Harvard, katika ripoti ya hivi karibuni kwa Umoja wa Matai kiljlijiunga na jumuiya ya kimataifa kwa kutambua tabia ya ubaguzi wa rangi ya utawala wa Kizayuni.

Ripoti hiyo kwa Kamisheni Huru ya Umoja wa Mataifa inayochunguza jinai za Israel na chimbuko la mzozo wa Palestina inabainisha sheria na kanuni za kibaguzi zinazotekelezwa na utawala haramu wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambao unawabagua kimfumo Wapalestina na kukandamiza haki zao za kiraia na kisiasa.

Ripoti ya pamoja ya kurasa 22 iliyopewa jina la ‘Apartheid Katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu: Uchambuzi wa Kisheria wa Vitendo vya Israel’ ambayo ilitolewa kwa ushirikiano na Jumuiya ya Usaidizi wa Wafungwa na Haki za Binadamu ya Addameer, imegundua kuwa mienendo ya utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ni sawa na jinai ambazo zilikiuka marufuku ya ubaguzi wa rangi.

 

Ripoti hiyo ya Februari 28, 2022, inaangazia mfumo unaotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina hasa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, "inagundua kwamba hatua za Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ni ukiukaji wa marufuku ya ubaguzi wa rangi na ni sawa na uhalifu wa ubaguzi wa rangi chini ya sheria za kimataifa.

Ripoti hii inaeleza kuwa utawala wa Tel Aviv unawanyima Wapalestina haki zao za kiraia na kisiasa kinyume na sheria za kimataifa.

Mbali na Harvard, wasomi wengine, Wapalestina na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, watetezi wa haki za kiraia, pamoja na sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa, wamekuwa wakilaani tabia ya ubaguzi wa rangi ya utawala wa Israel kwa miongo kadhaa.

Makundi yalikuwa yakitoa wito kwa viongozi na mashirika ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya Tel Aviv kwa jinai zake za wazi, kutokujali na kiburi katika kushughulika na Wapalestina na taasisi za kimataifa zinazotetea haki zao za kibinadamu zisizoweza kubatilishwa.

Hatimaye, mwezi Mei 2021 Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel ilianzishwa na Baraza la Haki za Kibinadamu, lililopewa jukumu la kuchunguza jinai za Israel, "ukiukaji na unyanyasaji" katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Zaidi ya hayo, Tume ya Umoja wa Mataifa itachunguza “sababu kuu za mivutano ya mara kwa mara, kukosekana kwa utulivu na uendelezaji wa migogoro, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kimfumo na ukandamizaji kwa misingi ya utambulisho wa kitaifa, kikabila, rangi au kidini” katika nchi zinazokaliwa kwa mabavu.

3478240

captcha