IQNA

Qur’ani Tukufu Inakabiliana na Ubaguzi wa Rangi/1

Kuzorota na Kudidimia Fikra

23:18 - December 23, 2023
Habari ID: 3478080
IQNA - Kutafakari kunaweza kuzingatiwa kama kigezo cha kutathmini maendeleo au kurudi nyuma kwa jamii.

Jamii inayojitenga na njia ya fikra na busara itagonga mwamba.

Moja ya matokeo ya ubaguzi wa rangi katika jamii ni kuzorota kwa uwezo wa kutafakari na  busara. Mfano mmoja wa ubaguzi wa rangi ni miongoni mwa Wayahudi wanaoamini kwamba Wayahudi hawapaswi kuchanganyika na wengine.

Kulingana na maoni yao, Bani Isra'il ni bora kuliko watu wengine wote duniani. Ndiyo maana wanaruhusu kuwepo ubaguzi rasmi kati ya Wayahudi na wengine katika kanuni za kijamii na hata jinsi watu wanavyotendewa.

Nadharia potovu ya etu watu bora na wateule, kiongozi bora na mteuli, nk daima imesababisha matokeo mabaya.

Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'an Tukufu anakataa madai kama hayo ya ubora:

 Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni. (Aya 1 ya Surat An-Nisaa)

Kwa hiyo watu wote ni vizazi vya wazazi sawa na hakuna watu au kikundi kilicho na ubora juu ya wengine.

Qur’ani Tukufu pia inasema: “Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.” (Aya ya 26 ya Surah Al-Hijr)

Kwa hiyo Mwenyezi Mungu anaposema watu wote wameumbwa kutokana na kitu kimoja (udongo), hakuna maana ya kudai ubora juu ya mtu mwingine kwa kuzingatia rangi au kabila.

Mwenyezi Mungu anakataa mawazo hayo yasiyo sahihi (ya ubora wa jamii moja juu ya nyingine), na Anawahimiza wanadamu wote kutafakari na kuanzisha kutafakari kuwa kizuizi dhidi ya kupotoka kwa mawazo.

Kwa hivyo kutafakari na busara ndio msingi wa ukuaji na maendeleo ya jamii. Hivyo basi ubaguzi wa rangi, ambao msingi wake ukosefu wa kutafakari na busara, unaweza kuchukuliwa kuwa sababu ya jamii kurudi nyuma.

Mwenyezi Mungu amekataa ubaguzi wa rangi kwa kuwakumbusha watu kwamba wote wameumbwa kutokana na kitu kimoja.

Habari zinazohusiana
captcha