IQNA

Kudhibiti nafsi, njia ya kweli ya kufikia ucha Mungu + Video

12:38 - April 14, 2022
Habari ID: 3475126
TEHRAN (IQNA)- Katika mfululizo wa darsa zake kuhus 'Katika Njia ya Kumhudumia Allah', mwanazuoni maarufu wa masuala ya akhlaqi nchini Iran Sheikh Dkt. Morteza Aghatehrani anazungumza kuhusu kudhibiti nafsi.

Sheikh Aghatehrani anasema mwanadamu huanza kupata uwezo wa kudhibiti nafasi yake akiwa na umri wa miezi mitano ambapo kwa mfano huweza kudhibiti mikono yake ingawa uwezo huo huwa dhaifu katika kipindi hicho cha awali.

Anasema baadhi ya wanasaikolojia wamejadili kadhiia hii kwa kina na mfano wao ni Jean Piaget. Anaongeza kuwa wakati mwanadamu anapofika umri wa miaka mitano uwezo wa kudhibiti afsi yake hupata nguvu zaidi. Akiwa katika umri huo huweza kudhibiti tabia na maneno yake lakini hilo linataka mazoezi makubwa.

Msomi huyo maarufu anasema kuna watu ambao hukariri makossa kwa sababu hushindwa kujizuia na hilo hutokana na kokosa kufanya mazozi ya kudhibiti nafsi. Anaongeza kuwa kwa mfano iwapo mtu ni mnafiki hutokana na kuwa alianza kuahdaa mara moja, ya pili nay a tatu na uovu huo ukawa ni ada. Mkabala wa hilo pia iwapo mwandamu atazoea kuwa mkweli na muaminifu basi jambo hilo litakuwa ni ada kwake.

Kwa msingi huo mwandamu anapaswa kujielimisha kuhusu kudhibiti nafsi yake na awe na azma ya kufanikisha nia yake njema. Kadiri mwanadamu anavyofanikiwa kudhibiti nafsi yake ndivyo anavyozidi kuimarika na kuwa na akhlaqi njema na anaweza kuwa ni mujahid au mlinganiaji kwa njia ya Allah SWT.

3478445

captcha