IQNA

Mawaidha

Kujidhibiti kwa Mtazamo wa Qur'ani

16:22 - January 18, 2024
Habari ID: 3478209
IQNA - Qur'ani Tukufu ina amri na maagizo mengi yanayolenga kusaidia ukuaji wa kiroho wa wanadamu.

Kujidhibiti ni aina ya usimamizi wa mtu mwenyewe. Inafafanuliwa kama uwezo wa kufuata matamanio ya yanayokubalika,  na kuchelewesha utimilifu wa hamu inayokubalika kijamii. Kwa mujibu wa mafundisho ya dini, kuidhibiti nafsi wakati fulani kunadhihirika katika kuacha madhambi na wakati mwingine katika kutekeleza faradhi za kidini na matokeo yake ni Taqwa (kumcha Mungu).

Wakati mwingine huonyeshwa katika kukabiliana na ugumu wa maisha na wakati mwingine katika kuishi pamoja kijamii, na katika hali zote mbili husababisha subira na ujasiri.

Aayah nyingi za Qur'ani Tukufu kuhusu kujidhibiti zinahusiana na Nafs (nafsi) na moyo. Moyo ndio unaopaswa kuwa makini na kujitawala wenyewe ili kuepuka kupotea. Matokeo ya ukosefu wa kujidhibiti humdhuru mtu mwenyewe.

Qur'ani Tukufu inasema katika Aya ya 164 ya Surah Al-Ana’am: “Matendo yote maovu ya mtu ni juu ya nafsi yake.

Kwa ujumla, kila mtu atajibu tu yanayomhusu  na hakuna atakayebeba mzigo wa mtu mwingine.

Qur'ani Tukufu inaapa mara 11 katika Surah Ash-Shams kusisitiza kwamba kila nafsi imepewa elimu ya uovu na uchamungu. (Surah Ash-Shams, Aya ya 1-8)

Miongoni mwa maagizo hayo ni yale kuhusu tabia na mienendo ambayo inakuza au kudhoofisha kujidhibiti. Mtu akijifunza kuhusu mambo yanayosababisha kudhoofika kwa kujidhibiti, anaweza kuyaepuka.

Kwa hivyo kama mtu atatekeleza mafundisho ya Fitra (maumbile) na akaiweka Nafsi yake kuwa safi kwa kujidhibiti, basi atafanikiwa lakini si kama atashindwa kujizuia mbele ya maovu.

“Wale wanaozitakasa nafsi zao watapata furaha ya milele na wale walioziharibu nafsi zao bila ya shaka watanyimwa (furaha). (Aya 9-10 za Surah Ash-Shams)

Kujidhibiti ni uwezo wa kudhibiti na kuangalia tamaa na kuweka utulivu katika uso wa tamaa au katika hali mbaya.

Kwa mujibu wa Imam Ali (AS), “Akili nyingi za utumwa zinatii matamanio makubwa kupita kiasi.” Na Qur'ani Tukufu inasema: “Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki??” (Aya ya 23  Surah Al-Jathiyah)

3486812

Kishikizo: qurani tukufu nafsi
captcha