IQNA

Sura za Qur’ani Tukufu /5

Miujiza ya Nabii Isa AS (Yesu) katika Surah Al-Ma'idah

22:44 - June 02, 2022
Habari ID: 3475328
TEHRAN (IQNA) – Sura tofauti za Qur’an zinarejelea kuzaliwa, maisha, miujiza, na maadui wa Nabii Isa (Yesu)-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake Sura ya tano ya Qur’ani inaashiria miujiza ya nabii huyu wa Mwenyezi Mungu.

Surah Al-Ma'idah ni Sura ya tano ya Quran na iliteremshwa Madina. Sura hiyo ina aya 120 na iko katika Juzi za 6 na 7 za Qur’ani Tukufu. Kwa mujibu wa mfuatano wa wahyi ulivyohusika, hii ni surah ya 113 ambayo Mtume Muhammad (SAW) aliipokea.

Aidha hii ni surah ndefu ya mwisho iliyoteremshwa katika miaka ya mwisho ya uhai wa Mtume.

Al-Ma'idah maana yake ni meza iliyowekwa kwa ajili ya kulia chakula na imetajwa katika aya za 112 na 114 za Surah Al Mai'dah.

"Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini." Al Mai'dah 112

"Akasema Isa bin Maryamu: Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku." Al Mai'dah 114

Al-Ma’ida inaashiria moja ya miujiza ya Nabii Isa AS ambayo ilikuja kufuatia ombi la wanafunzi wake. Walimwamini Nabii Isa AS lakini walitaka kuimarisha imani yao kwa kushuhudia muujiza. Kwa hiyo, Nabii Isa AS alimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ateremshe meza ya vyakula kutoka mbinguni.

Zaidi ya kuzaliwa na miujiza ya Nabii Isa AS, Surah hii pia inarejea kwenye hadithi nyingine kama vile Waisraeli kuvunja ahadi zao, kuuawa kwa Habil na Qabil, na Ghadir Khum.

Zaidi ya hayo, sura inazungumzia pia imani za Kiislamu, elimu, majukumu ya kidini kama vile wudhu (udhu), utekelezaji adhabu ya kifo, na adhabu ya wizi.

Moja ya sifa za Surah hii ni kutilia mkazo wake juu ya suala la Taqwa au kumcha Mwenyezi Mungu. Maneno "mcheni Mwenyezi Mungu" yamerudiwa mara 12 katika Surah Al Ma’idah, zaidi ya sura nyingine yoyote. Msisitizo huu wa Taqwa ni kwa sababu wanadamu wanapopata mali na cheo kizuri, kwa kawaida humsahau Mungu na kujihusisha na mambo ambayo yanawaharibia sifa, yanayokiuka ahadi, na kuharibu maadili ya jamii.

Habari zinazohusiana
captcha