IQNA

Surah za Qur'ani / 7

Suurat Al-A'raaf; Taswira ya deni la mwanadamu kwa Mwenyezi Mungu

15:26 - June 05, 2022
Habari ID: 3475339
TEHRAN (IQNA)- Mawazo na nadharia tofauti zimeelezwa kuhusu uumbaji wa mwanadamu na ulimwengu, lakini kwa mtazamo wa Kiislamu, Mwenyezi Mungu aliumba ulimwengu mzima na wanadamu katika kipindi fulani na wakati maalum; Kwa mujibu wa Uislamu, mwanadamu ameweka agano na Mwenyezi Mungu kabla ya kuumbwa awe khalifa au mrithi wa Mwenyezi Mungu katika ardhi.

Sura ya saba ya Qur'ani Tukufu inaitwa " Al-A'raaf " ambayo pamoja ina aya 206 imejumuishwa katika juzuu za nane na tisa za Qur'ani; Suurat Al-A'raaf iliteremshwa kwa Mtume Muhammad SAW wakati Waislamu wakiwa katika hali ngumu, yaani, wakati wa mzingiro wa kiuchumi huko Makkah.

Suurat Al-A'raaf, kama surah zingine za Makkah, inazungumzia mada za uumbaji, uthibitisho wa Tauhidi, mapambano dhidi ya ushirikina, na ubainishaji wa nafasi ya mwanadamu katika ulimwengu. Pia, ili kuonyesha matokeo ya upotofu kutoka kwenye njia ya Tauhidi, inahusika na historia ya makabila au kaumu na Manabii waliotangulia kama vile Nuhu (AS), Lut (AS) na Shoaib (AS).

 

Mada kuu za Suurat Al-A'raaf zinaweza kuorodheshwa kama ifuatavyo:

Uumbaji wa Mwanadamu

Sura hii inazungumzia kwa kina kuhusu kuumbwa kwa Adam na Hawa, wanadamu wawili wa kwanza, walivyofitiniwa na kuhadaiwa shetani na kuondoka kwao peponi, na jinsi walivyoanza maisha yao duniani.

Kujikurubisha na Qur'ani

Qur'ani Tukufu inatajwa kuwa ni kitabu kitakatifu kwa ajili ya mwongozo na rehema maalum za Mwenyezi Mungu kwa walimwengu, na inaiita Siku ya QIyama kuwa ni siku ya kudhihiri tafsiri ya Qur'ani.

Mwanzo wa kuumbwa ardhi na mbingu

Kwa mara nyingine tena, inaeleza mwanzo wa kuumbwa mbingu na ardhi, na inabainisha uwongofu na upotofu wa wanadamu kuhusiana na Mola wao Mlezi.

Hadithi ya Nabii Musa AS

Hadithi ya Nabii Musa AS pia imeelezwa kwa kina katika surah hii. Kwanza inashughulika na matukio yaliyotokea baina yao na Firauni, na kisha inaeleza “tabia ya wana wa Israeli” na Musa AS

Maagano ya Mwenyezi Mungu

Vile vile inakumbusha maagano yaliyowekwa kati ya mwanadamu na Mwenyezi Mungu na kumfanya mwanadamu awajibike kuhusu ushirikina na imani yake, na katika suala hili, hadithi zinasimuliwa kuhusu juhudi za mitume kuwaongoza watu.

Akhera

Mada ya Siku ya Qiyama ni suala jengine lililotajwa katika surah hii; Suala ambalo hakuna mtu ila Mungu anajua.

Habari zinazohusiana
captcha