IQNA

Taazia

Qari Mwandamizi wa Misri, Abdul Rahim Dawidar Afariki Dunia

20:05 - October 24, 2023
Habari ID: 3477780
CAIRO (IQNA) – Sheikh Abdul Rahim al-Dawidar, qari wa Qur’ani Tukufu na msomaji wa Ibtihal nchini Misri, alifariki akiwa na umri wa miaka 86.

Katika miaka ya karibuni, alitambuliwa kuwa msomaji mkuu wa Ibtihal katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Alizaliwa Machi 1937 huko Tanta, alipoteza baba yake akiwa na umri wa miaka 5 na kaka yake mkubwa alimlea.

Alianza kujifunza Qur’ani Tukufu katika umri mdogo, akifanya mazoezi ya kusoma Qur’ani Tukufu na Ibtihal chini ya usimamizi wa maustadhi maarufu Mohammad Naqshbandi, Mustafa Ismail na Taha al-Fashni.

Al-Dawidar alisafiri katika nchi nyingi za Kiislamu kwa ajili ya kusoma Qur’ani Tukufu na Ibtihal.

Alitembelea Iran mwaka 2013 na kuhudhuria programu za Qur'ani nchini humo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Pia alisoma Ibtihal wakati wa mkutano wa wasomaji Qur’ani Tukufu na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei.

Baadaye aliuelezea mkutano huo uliodumu kwa kwa muda wa saa nne, kuwa ni wa kipekee. Baada ya kurejea Misri, aliwasifu watu wa Iran kwa umakini wao wa kuhudhuria programu za Qur'ani Tukufu. Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo. Shughuli za Qur'ani hufanyika kwa wingi nchini humo ambapo wasomaji wakuu wa Qur’ani Tukufu wakuu wa ulimwengu wa Kiislamu ni Wamisri.

Kishikizo: misri Ibtihal
captcha