IQNA

Waliobobea

Sheikh Al-Hilbawi qari aliyekuwa na kipaji cha kipekee katika Ibtihal

20:47 - February 10, 2024
Habari ID: 3478328
IQNA – Muhammad Abdul Hadi Muhammad al-Hilbawi alizaliwa katika wilaya ya Bab al-Sharia mjini Cairo mnamo Februari 9, 1946, alianza kuhifadhi Qur’ani Tukufu akiwa mtoto chini ya uongozi wa babu yake.

Alifuata mitindo ya qiraa ya Sheikh Mohammad Rafat na Ali Mahmoud, na mitindo ya Ibtihal ya Zakaria Ahmad na Taha Al-Fashni, mpaka akakuza sauti yake ya kipekee.

Alisafiri katika nchi mbalimbali na kwa ajili ya kusoma Qur’ani Tukufu na Ibtihal.

Alipata tuzo kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri kwa miaka yake ya kujitolea na mazoezi katika kusoma Qur'ani Tukufu na Ibtihal.

Pia alibobea katika muziki wa Kiarabu kutoka kwa walimu bora katika nyanja hii. Alijifunza kutoka kwa wasomaji wa Enzi ya Dhahabu ya Misri mwishoni mwa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, na mnamo 1929 alipata usomaji Qur’ani Tukufu na Ibtihal kwenye Redio ya Qur'ani ya Misri.

Ustadh Sheikh Muhammad Abdul Hadi Muhammad Al-Hilbawi, ambaye alikuwa na kisukari kwa muda mrefu, alifariki usiku wa Juni 15, 2013, akiwa na umri wa miaka 67.

4198536

Kishikizo: Ibtihal qurani tukufu
captcha