IQNA

Waislamu Marekani

Marekani yashuhudia ongezeko kubwa la chuki dhidi ya Waislamu

14:17 - November 10, 2023
Habari ID: 3477872
WASHINGTON, DC (IQNA) - Ripoti mpya inasema kwamba matukio ya chuki dhidi ya Waarabu na Waislamu nchini Marekani yameongezeka hadi kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu vita kati ya Israel na Wapalestina kuzuka katika Ukanda wa Gaza mwezi uliopita.

Ripoti hiyo, iliyotolewa Jumatano na Baraza la Mahusiano ya Kiislamu ya Marekani (CAIR), kundi la Waislamu la kutetea haki za kiraia , inasema kwamba ilipokea maombi 1,283 kutoka kwa Waislamu waliotaka usaidizi na za chuki dhidi ya Waislamu kutoka Oktoba 7 hadi Novemba 4, ikiwa ni ongezeko la 216% kuongezeka kutoka wastani wa kila mwezi wa 406 katika 2022.

Ripoti hiyo inasema kuwa matukio hayo yalihusisha Wamarekani wa rika na asili mbalimbali, wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi, waandamanaji na madaktari, pamoja na misikiti kote Marekani.

Mkurugenzi wa utafiti wa CAIR, Corey Saylor, alisema katika taarifa yake kwamba kuongezeka kwa ubaguzi kunachochewa na "maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na Palestina" ambayo yalitumiwa kuhalalisha mauaji ya Wapalestina wasio na ulinzi huko Gaza na kuwanyamazisha wafuasi wa haki za binadamu za Palestina nchini Marekani.

Alisema Waislamu wa Marekani wanakabiliwa na wimbi kubwa zaidi la chuki dhidi ya Uislamu tangu mgombeaji wa wakati huo Donald Trump alipotangaza pendekezo lake la kupiga marufuku Waislamu mnamo Desemba 2015.

Ripoti hiyo pia inataja matukio yaliyoripotiwa hadharani ya chuki dhidi  Waislamu au Wapalestina, kama vile kifo cha kuchomwa kisu cha mtoto wa miaka 6 Wadea Al-Fayoume, mvulana Mpalestina-Mmarekani kutoka Chicago, Oktoba 15, katika tukio la uhalifu wa chuki. Mamake pia alijeruhiwa katika shambulio hilo na mwenye nyumba wao. Matukio mengine ni pamoja na majaribio ya mauaji, vitisho vya vurugu, mashambulizi ya magari na ghasia za bunduki dhidi ya waandamanaji wanaounga mkono Palestina.

Saylor alitoa wito kwa Rais Biden kuishinikiza Israel isitishe mapigano huko Gaza na kusema kuwa vita nje ya nchi hunachangia machafuko na chuki ndani ya Marekani.

3485946

Habari zinazohusiana
captcha