IQNA

Jiografia ya Matukio katika Qur'ani Tukufu/4

Kisa cha Nabii Suleman na Mji Mkuu wa Ufalme Wake

10:38 - December 18, 2023
Habari ID: 3478051
IQNA – Upeo wa utawala wa Mtume Suleiman (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) ulikuwa mkubwa kiasi kwamba hata falme kubwa zaidi katika historia zinaonekana kuwa ndogo ikilinganishwa ufalme wa nabii huyo.

Ufalme wake ulikuwa mkubwa na wenye nguvu kiasi kwamba si wanadamu tu, bali viumbe vyote vilimtii.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 15-17 ya Surah An-Naml:

Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini.  Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri (kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo yakapangwa kwa nidhamu.

Suleman (AS) alikuwa na ufalme wenye nguvu zaidi duniani na alifanikisha hilo baada ya kumwomba Mungu: “Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji."  (Aya ya 35 ya Surat Saad)

Suleiman (AS) alitawala watu, majini, wanyama na hata upepo. Chochote alichotaka, majini wangemtengenezea.

Siku moja, ndege aitwaye Hudhud alimjulisha Suleiman kwamba amempata mwanamke anayeabudu jua anatawala juu ya watu wa Yemen. Sulemani alimwandikia barua mtawala huyo na kumsihi amtii. Ili kuepusha vita, mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Malkia wa Saba (Sheba), alimpelekea zawadi lakini Sulemani hakuipokea. Kwa hiyo alianza safari ya kukutana na Sulemani katika mji wake mkuu. Sulemani akauliza, “Ni nani awezaye kuleta kiti chake cha ufalme kwangu kabla hajafika hapa?” Mmoja wa majini alisema angeweza kufanya hivyo kabla ya Suleiman hatua moja kwa mguu. Mwingine alisema angeweza kumletea kabla ya kupepesa kope.

Baada ya Malkia wa Saba kufika na kuona hivyo, pamoja na matukio mengine, alianza kumwamini na kumtii Sulemani.

Mji mkuu wa ufalme wa Suleiman ulikuwa mji mtakatifu wa al-Quds(Jerusalem). Al-Quds ni mji wa tatu kwa utakatifu kwa Waislamu na pia ni mahali patakatifu kwa Wayahudi na Wakristo. Mji ulianza kusitawi wakati wa falme za Daudi (AS) na Sulemani (AS).

Kishikizo: qurani tukufu suleiman
captcha