IQNA

Sura za Qur'ani Tukufu /111

Taswira ya hatima ya maadui wa Uislamu katika Sura Al-Masad

12:06 - September 03, 2023
Habari ID: 3477540
TEHRAN (IQNA) - Kumekuwepo na visa vya kuvunjiwa heshima kwa Qur'ani Tukufu katika nchi za Magharibi katika mwezi wa hivi karibuni, na kusababisha malalamiko na hasira miogoni mwaWaislamu duniani kote.

Wale vitendo hivyo vya kufuru kwa hakika wataadhibiwa vikali na Mwenyezi Mungu. Na hivi ndivyo Qur'ani Tukufu imesisitiza, ikiwa ni pamoja na katika Surah Al-Masad.

Al-Masad ni Sura ya 111 ya Qur'ani Tukufu ambayo ina aya 5 na iko katika Juzuu ya 30.

Ni Makki na ni Sura ya 6 iliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Inaitwa al-Masad, kwa sababu neno al-Masad (nyuzi zilizosokotwa au nyuzi za mitende) linakuja katika aya ya mwisho.

Sura hii iliteremshwa wakati Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) alipoanza mwaliko wake wa wazi wa kuwaita watu kukumbatia Uislamu. Sura yote inamhusu mtu anayeitwa Abu Lahab na mkewe.

Inazungumza juu ya kile walichokifanya, ukweli kwamba wataangamia, na adhabu inayowangojea motoni.

Hii ndio sura pekee ya Qur'ani Tukufu ambayo mmoja wa maadui wa Uislamu ametajwa wa jina.

Maudhui ya Sura yanaonyesha kwamba Abu Lahab na mkewe walionyesha uadui mkubwa dhidi ya Uislamu na walimsumbua Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kwa njia tofauti.

Wawili hao walikuwa miongoni mwa maadui maalum wa Mtume Muhammad (SAW) na walitumia pesa nyingi kuzuia kuenea kwa Uislamu. Ndio maana Sura inawalaani. Baadhi ya wafasiri wanaamini kuwa laana si ya wawili hao pekee bali inaeleza hatima ya maadui wa Uislamu kwa ujumla na Abu Lahab na mkewe wametajwa kuwa mifano au nembo ya maadui.

Sura inamwita Ummu Jamil, mke wa Abu Lahab, kama mchukua kuni. Kuna maoni tofauti kati ya wakalimani kuhusu hili. Mtazamo mmoja ni kwamba alikusanya miiba kutoka jangwani na kuiweka kwenye njia ya Mtume Muhammad (SAW).

Maelezo mengine kwa mke wa Abu Lahab ni kwamba " Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa!" (Aya ya  5)

Wafasiri wengine wanasema hii ni juu ya maisha yake katika ulimwengu huu. Wakati wanawake wengine walikuwa na mkufu uliotengenezwa kwa dhahabu, mke wa Abu Lahab alikuwa na mkufu mmoja uliotengenezwa kwa nyuzi za mitende, ambayo kwa namna fulani ni mtazamo wa dharau kwake.

Baadhi ya wengine wanasema inaonyesha jinsi atakavyoingia motoni na huo ni mfano wa hatima ya wanaume na wanawake ambao wanachukia Uislamu waziwazi.

Kishikizo: SURA ZA QURANI
captcha